Hapo mwanzo, Mungu alinena Neno, na ulimwengu ukapata kuwepo. Neno hilo hilo linakungoja hapa katika kila kitabu cha Biblia, kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo, huru kusoma na huru kusikia likisomwa kwa sauti.
Hapo mwanzo alikuwako Neno, naye huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu. Vitu vyote viliumbwa kupitia kwake, na hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa pasipo yeye. Ndani yake kulikuwa na uzima, nao huo uzima ulikuwa nuru ya watu. Nuru hungʼaa gizani nalo giza halikuishinda. (Yohana 1:1-5)
Habari Njema
Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele. Maandiko haya ndio yanayonishuhudia mimi. — Yohana 5:39
Naye akianzia na Sheria ya Musa na Manabii wote, akawafafanulia jinsi Maandiko yalivyosema kumhusu. — Luka 24:27
Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli. — Yohana 1:14
“Lakini wewe, Bethlehemu Efrata, ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli, ambaye asili yake ni kutoka zamani, kutoka milele.” — Mika 5:2
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa. — Yohana 3:16-17
Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.” — Luka 19:10
Kisha Yesu akasema nao tena, akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu yeyote akinifuata, hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.” — Yohana 8:12
kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, — Warumi 3:23
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. — Warumi 6:23
Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu. — Warumi 5:8
Lakini alijeruhiwa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu; adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona. Sisi sote, kama kondoo, tumepotea, kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, naye Bwana aliweka juu yake maovu yetu sisi sote. — Isaya 53:5-6
Ndani yake tunao ukombozi kupitia kwa damu yake, yaani msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake — Waefeso 1:7
“Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha katika nafsi zenu. Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.” — Mathayo 11:28-30
“Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. — Yohana 10:11
Nao uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe uliye Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. — Yohana 17:3
Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu. — Yohana 14:6
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kupitia kwa imani, nayo haikutokana na ninyi wenyewe. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, si kwa matendo, ili mtu yeyote asije akajisifu. — Waefeso 2:8-9
Bali wote waliompokea, yaani wale walioliamini jina lake, aliwapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu. — Yohana 1:12
Tazama! Nasimama mlangoni nabisha. Kama mtu yeyote akisikia sauti yangu na kufungua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami. — Ufunuo 3:20
Kwa maana, “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokolewa.” — Warumi 10:13
“Lakini yule mtoza ushuru akasimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni, bali alijipigapiga kifuani na kusema: ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’ — Luka 18:13
Kwa sababu, ukikiri kwa kinywa chako kwamba “Yesu ni Bwana,” na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. — Warumi 10:9
Vitabu vya Agano la Kale katika Biblia ya Sauti ya Kiswahili
Vitabu vya Agano Jipya katika Biblia ya Sauti ya Kiswahili
Maneno muhimu:
Biblia ya sauti ya Kiswahili
Biblia ya sauti
Biblia ya Kiswahili
Neno Bibilia Takatifu
Biblia Takatifu Kiswahili
Biblia ya sauti bila malipo
Biblia bure
sikiliza Biblia
sikiliza neno la Mungu
soma Biblia
soma Biblia mtandaoni
Biblia mtandaoni
neno la Mungu
pakua Biblia
pakua Biblia ya Kiswahili
Biblia ya sauti mp3
Biblia mp3 Kiswahili
Biblia nje ya mtandao
Biblia offline Kiswahili
Agano la Kale
Agano Jipya
Habari Njema
Injili
Biblia kamili ya Kiswahili
Biblia ya sauti ya bure
kusikiliza Biblia kwa sauti
Biblia ya kusikiliza
Neno la Mungu kwa sauti
Biblia ya simu
programu ya Biblia ya Kiswahili
mistari ya Biblia
Mwanzo hadi Ufunuo
Biblia kwa Kiswahili
usome Biblia
Biblia ya dijitali
Neno NEN
Kiswahili Biblia ya sauti
sala na neno la Mungu
Biblia ya Kikristo Kiswahili